Habari Rfi-ki

  • Autor: Vários
  • Narrador: Vários
  • Editor: Podcast
  • Duración: 3:47:31
  • Mas informaciones

Informações:

Sinopsis

Makala ya kila siku yanayompa fursa msikilizaji kutoa maoni yake juu ya habari zilizopewa uzito wa juu kwa siku husika. Msikilizaji hushiriki kwa kutuma ujumbe mfupi pamoja na kupiga simu.

Episodios

  • Ajali za boti katika mataifa ya Afrika yakiwemo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo

    24/09/2024 Duración: 10min

    Watu wengi wameendelea kupoteza maisha katika majanga ya majini

  • Mwanae rais wa Uganda Jenerali Muhoozi asema nchi hiyo itaongozwa na polisi au jeshi

    23/09/2024 Duración: 10min

    Jenerali Muhoozi Kainerugaba, amesema hatowania urais ila Uganda itaendelea kuongozwa na polisi au jeshi baada ya rais Museveni Juma lililopita mtoto wa Rais wa #Uganda pia  mkuu wa majeshi Jenerali Muhoozi Kainerugaba, kuwa  nchi hiyo itaongozwa na mwanajeshi au polisi baada ya baba yake kuondoka madarakani.

  • Tanzania: Rais Samia awaonya mabalozi

    19/09/2024 Duración: 09min

    katika makala  haya  tunajadailki hatua ya rais wa rais wa #Tanzania #SamiaSuluhuHassan , kuwaonya makutoa ya pamoja  taarifa kulaani matukio ya utekaji na mauaji dhidi ya wakosoaji wa Serikali yake.  Je unafikiri kauli Samia ni sahihi?Ndilo swali tumekuuliza, na haya hapa baadhi ya maoni yako.

  • Africa : Ukosefu wa ajira wachangia uhalifu miongoni mwa vijana

    18/09/2024 Duración: 09min

     Katika makala haya tunajadili kinachoendelea katika mataifa mengi ya  Afrika kuendelea kushuhudia ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana, hii likichangia kwa kiasi kikubwa uhalifu. Je Wewe unafanya nini ili kupata riziki ya kila siku ?Ndilo swali tumekuulizaHaya hapa baadhi ya maoni yako.

  • Africa : Ndoa zinaendelea kuvunjika haraka kinyume na awali

    17/09/2024 Duración: 09min

    Katika makala haya tunajadili misururu ya kuvunjika kwa ndoa za siku hizi  hili haliathiri tu watu wa kawaida  bali pia  watu maarufu katika jamii zetu. Je unafikiri nini kinachangia ndoa za siku hizi kuendelea kuvunjika haraka kinyume na zamani?Ndilo swali tumekuuliza, na haya hapa baadhi ya maoni yako.

  • Sudan Kusini : Serikali yaarisha uchaguzi kutokana na shinikizo za wadau

    16/09/2024 Duración: 09min

    katika makala haya tunajadili hatua ya serikali ya Sudan Kusini juma lililopita kutangaza kuahirisha uchaguzi mkuu uliokuwa ufanyike mwezi Desemba mwaka huu. Uchaguzi huu sasa ukisongezwa mbele kwa miaka miwili baada ya shinikizo la ndani na nje.Je huu ni uamuzi sahihi kwa Sudan Kusini?Haya hapa baadhi ya maoni yako

  • Kila Ijumaa rfi Kiswahili inakupa nafasi kuchangia chochote kile

    01/09/2024 Duración: 10min

    Kila ijumaa inapata nafasi kuchangia mada yoyoyte ndani ya makala Habari Rafiki, makala ambayo huenda hewani ndani ya rfi Kiswahili kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa. Skiza kufahamu maoni ya waskilizaji kuhusiana na mada mbalimbali.

  • Sudan : UN yatathimini kutangaza vikwazo dhidi ya majenerali wa Sudan

    29/08/2024 Duración: 09min

    Katika makala haya tunajadili hatua ya umoja wa mataifa kusema unatathimini kutangaza vikwazo dhidi ya majenerali wawili nchini Sudan ambao wamekuwa kwenye vita kwa zaidi ya miezi 17. Je unafiriki kutangazwa kwa vikwazo dhidi ya majenerali wa Sudan kutasitisha vita nchini Sudan? Unahisi jumuiya ya kimataifa imesaidia, kutatua mizozo Africa, ndio maswali tumekuuliza. Haya hapa baadhi ya maoni yako.

  • Kenya : Mataifa ya Africa yakosa kuzingatia katiba

    28/08/2024 Duración: 09min

    Kwenye makala ya Habari Rafiki leo tunajadili kilichofanyika nchini Kenya, ambapo taifa hilo la Africa mashariki limeadimisha miaka 14 tangu lijipatie katiba ya mwaka 2010, ila imekuwa vigumu kwa serikali kutekeleza baadhi ya vipengee vya katiba hiyo. Unafiriki nini huzuia serikali yetu kuttotekeleza  katiba?Ndilo swali tumekuuliza, na haya maoni yako.

  • Africa : Inasubiri chanjo ya Mpox kutoka ulaya

    27/08/2024 Duración: 09min

     katika makala ya Rabari Rafiki, leo mskilizaji tunajadili hatua ya Mataifa ya Afrika yalioathirika na ugonjwa Mpox kuendelea kusubiri chanjo kutoka kwa mataifa ya magharibi ili kuwapa raia walioathirika.  Je unafikiri kwa nini hadi sasa Afrika haiwezi tegeneza chanjo yake? Ndilo swali tumekuuliza na haya maoni yako.

  • Sudan : Kiongozi wa kijeshi asema yuko tayari kwa vita na hatashiriki mazungumzo ya amani

    26/08/2024 Duración: 09min

    Katika makala haya tunajadili  hatua ya kiongozi wa kijeshi nchini Sudan, kusema hataki mazungumzo yoyote yatayohusisha wapiganaji wa RSF, akisema jeshi liko tayari kupigana hata kwa miaka 100. Matamshi yake yamekuja wakati huu Marekani ikiongoza juhudi za kupata mwafaka wa mani kati yake na vikosi vya RSF.

  • Matukio ya watuhumiwa kutoroka wakiwa katika vituo vya polisi na jela

    22/08/2024 Duración: 09min
  • Juhudi za kukabili unyanyapaa dhidi ya watu wanaoishi na virusi vya ukimwi

    20/08/2024 Duración: 09min

    Unyanyapaa ni hali inayowakumba watu wengi wanaoishi na virusi vya HIV katika mataifa ya ukanda.

  • Migogoro na ukosefu wa amani katika nchi wanachama za jumuia ya SADC

    19/08/2024 Duración: 09min
  • Siku ya kimataifa ya kupiga vita biashara haramu ya binadamu

    31/07/2024 Duración: 09min

    Wataalamu wanasema biashara hii haramu imekuja na mfumo mpya wa watu kusafirishwa kutafutiwa ajira katika mataifa ya kigeni.

  • Serikali ya DRC, imetangaza kuanza kuwaachia baadhi ya wafungwa kutoka katika jela zake

    29/07/2024 Duración: 10min
  • Mtazamo wa msikikilizaji kuhusu mawaziri kutoka upinzani kuunda serikali

    25/07/2024 Duración: 10min

    Rais William Ruto amependekeza viongozi wanne kutoka chama cha ODM cha Raila Odinga kuwa mawaziri Miongoni mwa viongozi hao ni Ali Hassan Joho ,John Mbadi ,Wicliffe Oparanya na Opiyo Wandayi

  • Mtazamo wa msikililizaji kuhusu maandamano Kenya iwapo yameathiri nchi zingine

    25/07/2024 Duración: 10min

    Vijana nchini Kenya wamekuwa wakiongoza maandamano dhidi ya serikali ya rais William Ruto Nchi ya Uganda imeshuhudia pia maandamano ,yanayoongozwa na vijana wa Gen Z kupinga ufisadi na maovu mengine

  • Maoni yako kuhusu matukio ya juma hili

    19/07/2024 Duración: 09min

    Kila Ijumaa rfi kiswahili inakupa nafasi kuchangia  chochote kile ambacho umeskia kwenye matangazo yetu au yale yanayoendelea hapo uliopo. Juma hili waskilizaji wetu walikuwa na maoni mseto kuhusu matukio yanayoendelea kushuhudiwa duniani. Kufahamu mengi skiza makala haya.

  • Mtazamo wa msikilizaji kuhusu kuchaguliwa tena kwa rais Paul Kagame

    19/07/2024 Duración: 10min

    Tume ya uchaguzi ya Rwanda imethibitisha Paul Kagame ni mshindi wa uchaguzi wa Julai 15 ambapo alipata asilimia 99.18 ya kura zote

página 1 de 2