Gurudumu La Uchumi

Informações:

Sinopsis

Fahamu masuala kadha wa kadha kuhusu uchumi kama vile, namna ya kupambana na umaskini, mfumuko wa bei, kushamiri kwa matumizi ya dola na athari za kuyumba kwa uchumi wa dunia kwa nchi za Afrika. Mada hizi zinafanyiwa utafiti wa kina na zinazungumzwa kwa lugha rahisi inayoeleweka ili kukufanya uelewe na usichoke kusikiliza .

Episodios

  • Ujuzi kwa vijana na teknolojia

    12/07/2023 Duración: 10min

    Makala ya Gurudumu la uchumi juma hili, inaangazia siku ya "ujuzi kwa vijana duniani' inayoadhimishwa kila tarehe 15 ya mwezi Julai kila mwaka, lengo ni kuwawezesha walimu, wakufunzi na vijana kutumia ujuzi wao kwa maendeleo.Leo mtayarishaji amezungumza na Tukupala Mwalyolo, msichana anayeunda ndege zisizo na rubani 'drone', pamoja na Emmanuel Cosmas Msoka, kijana mbunifu wote wakitumia teknolojia kutafuta suluhu na wako Tanzania.

  • Faida ya mfumo wa malipo ya pamoja barani Afrika

    31/05/2023 Duración: 09min

    Mwezi Januari mwaka 2022, benki kuu pamoja na wakuu wa nchi za umoja wa Afrika, waliunga mkono mchakato ulioanzishwa na benki ya Afrexim, ambayo ilitengeneza mfumo wa malipo uliolenga kurahisisha ufanyaji wa malipo na manunuzi kati ya nchi na nchi, mtu na mtu na biashara kwa biashara barani Afrika. Mfumo huu unafahamika kama Pan-African payments and Settlement System PAPSS, kwa kiasi kikubwa unapunguza changamoto ya ufanyaji malipo kwa kutumia fedha za kigeni kama Dola, ambapo kupitia mfumo huu nchi, biashara au watu wanaweza kubadilishana huduma kwa kutumia fedha ya nchi husika.Lakini je, ni kwanini bado mfumo huu hauonekani kutoa jibu kwa tatizo lililoko hasa linapokuja suala la malipo au ununuzi wa biadhaa ambapo nchi zinalazimika kutumia dola ? Mbali na hili tutaangazia pia ikiwa uongezaji wa tozo na kodi ndio suluhu kwa nchi nchi za Afrika kukabikliana na changamloto za kifedha na kiuchumi.Makala  ya Gurudumu la uchumi juma hili, inaenda kuangazia masuala haya kwa kina.

  • Changamoto za kilimo na suluhu endelevu kwa bara Afrika

    30/05/2023 Duración: 10min

    Mkutano wa kimataifa uliowakutanisha wakulima kutoka mataifa ya Afrika, Karibian na Pacific waliokutana nchini Rwanda ambapo walijadiliana kwa pamoja changamoto za kilimo ilizishugulikiwe na kupata suluhu endelevu.

  • Umuhimu wa bara la Afrika kuwa na mfumo wa pamoja wa kufanya malipo kidijiti

    17/05/2023 Duración: 10min

    Kwa mujibu wa umoja wa Mataifa, malipo ya kidijiti au ya kimtandao yanachangia pakubwa katika kujenga msingi imara wa kufikia maendeleo endelevu, kwanini? Ni kwasababu malipo haya yanapokuwa rahisi, salama, ya wazi na binafsi, yatawezesha ukuaji wa fursa kama nishati, maji na mikopo.Katika kipindi hiki utamsikia, Lucy Nshuti Mbabazi, kutoka taasisi ya umoja wa Mataifa ya muungano wa Better than Cash, Lacina Kone, mkurugenzi wa Smartafrica pamoja na Kwizela Aristide Basebya, mtafiti wa Teknolojia za Mawasiliano ya Umma na Matumizi yake serikalini, akiwa Beijing, China.

página 2 de 2