Gurudumu La Uchumi

Faida ya mfumo wa malipo ya pamoja barani Afrika

Informações:

Sinopsis

Mwezi Januari mwaka 2022, benki kuu pamoja na wakuu wa nchi za umoja wa Afrika, waliunga mkono mchakato ulioanzishwa na benki ya Afrexim, ambayo ilitengeneza mfumo wa malipo uliolenga kurahisisha ufanyaji wa malipo na manunuzi kati ya nchi na nchi, mtu na mtu na biashara kwa biashara barani Afrika. Mfumo huu unafahamika kama Pan-African payments and Settlement System PAPSS, kwa kiasi kikubwa unapunguza changamoto ya ufanyaji malipo kwa kutumia fedha za kigeni kama Dola, ambapo kupitia mfumo huu nchi, biashara au watu wanaweza kubadilishana huduma kwa kutumia fedha ya nchi husika.Lakini je, ni kwanini bado mfumo huu hauonekani kutoa jibu kwa tatizo lililoko hasa linapokuja suala la malipo au ununuzi wa biadhaa ambapo nchi zinalazimika kutumia dola ? Mbali na hili tutaangazia pia ikiwa uongezaji wa tozo na kodi ndio suluhu kwa nchi nchi za Afrika kukabikliana na changamloto za kifedha na kiuchumi.Makala  ya Gurudumu la uchumi juma hili, inaenda kuangazia masuala haya kwa kina.