Habari Za Un

Informações:

Sinopsis

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Episodios

  • UN: Wananchi wa Gaza wako katika jakamoyo wakisubiri taarifa kuhusu wito wa kusitisha mapigano

    01/05/2024 Duración: 01min

    Wakati kukiwa na ongezeko la wito wa kimataifa kwa Israel kujizuia na mashambulizi zaidi Gaza na ripoti za leo za mashambulizi mengine mabaya zaidi ya usiku kucha, wahudumu wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa wamesisitiza kuhusu athari mbaya zinazoendelea za vita hiyo na haja ya kuhakikisha njia za kuaminika za usambazaji wa misaada kwa watu wanaohitaji kwa udi na uvumba zinapatikana. Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula Duniani WFP ambapo kupitia mkurugenzi wake wa eneo linalokaliwa la Palestina Matthew Hollingworth, limesema "Theluthi moja ya familia zote zinazoishi hapa zina watoto wa umri wa chini ya miaka mitano, hao ni watoto wengi sana” Akizungumza kutoka shule ya Deir Al Balah, inayoendeshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina, UNRWA amesema watoto hawa wana mahitaji mengi “Wanachohitaji ni shule, maji safi na salama, utulivu zaidi,  na pia wanahitaji kurejea kwa maisha ya kawaida, "Likiunga mkono wasiwasi huo shirika la UNRWA limegusia masham

  • 01 MEI 2024

    01/05/2024 Duración: 09min

    Hii leo jaridani inaangazia hali ya kibinadamu Rafah ambapo wakimbizi wa ndani Gaza wako katika jakamoyo wakisubiri taarifa kuhusu wito wa kusitisha mapigano. Pia inamulika udhibiti wa taka za plastiki kambini Kakuma. Makala inaangazia jamii ya watu wa asili na mashinani inatupeleka nchini DRC, kulikoni?Wakati kukiwa na ongezeko la wito wa kimataifa kwa Israel kujizuia na mashambulizi zaidi Gaza na ripoti za leo za mashambulizi mengine mabaya zaidi ya usiku kucha, wahudumu wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa wamesisitiza kuhusu athari mbaya zinazoendelea za vita hiyo na haja ya kuhakikisha njia za kuaminika za usambazaji wa misaada kwa watu wanaohitaji kwa udi na uvumba zinapatikana.Katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma iliyoko kaskazini magharibi mwa Kenya, ambapo mkimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC amegeuza taka ngumu kuwa lulu na hivyo sio tu kuweka usafi kwenye makazi ya kambini, bali pia kuinua kipato chake na cha jamii inayomzunguka.Makala inaangazia changamoto za mabadiliko ya tabianchi z

  • UNHCR: Taka ngumu Kakuma zageuka lulu, wakimbizi vipato vyaongezeka

    01/05/2024 Duración: 01min

    Katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma iliyoko kaskazini magharibi mwa Kenya, mkimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC amegeuza taka ngumu kuwa lulu na hivyo sio tu kuweka usafi kwenye makazi ya kambini, bali pia kuinua kipato chake na cha jamii inayomzunguka.Ninapoona plastiki naona fursa za ajira! Ni kauli hiyo ya Raphael Bassemi, mkimbizi kutoka DRC akiwa hapa kambini Kakuma akizungumza huku wanawake na wanaume waliovalia maovaroli na glovu na barakoa wakiokota taka. Anasema anafurahi anapoona jamii inashiriki na zaidi ya yote wanawake wasiokuwa na ajira sasa wameajiriwa, "Nilipoanza nilijikita tu kwenye plastiki, lakini ilibainika kuwa kuna takangumu nyingi za kudhibitiwa. Sasa  ninajishughulisha na aina zote za taka.”Video ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi linaonesha taka mbalimbali zikiwemo mifupa ya mafuvu ya ng’ombe, vyuma, seng’eng’e na kadhalika. Sasa amesharejeleza tani zipatazo 100 za takangumu."Tunatengeneza rula kwa ajili  ya wanafunzi, vibanio vya ku

  • Mama akivaa kofia yake tunaweza kurejesha amani kuanzia katika familia hadi kimataifa: Adam Ole Mareka

    30/04/2024 Duración: 08min

    Mkutano wa 23 wa Jukwaa la Kudumu kuhusu Masuala ya Watu wa Asili, UNPFII limekunja jamvi mwishoni mwa wiki hapa Umoja wa Mataifa baada ya wiki mbiliza kujadili masuala mbalimbali  ikiwemo mchango wa jamii hizo katika kudumisha amani Adam Kulet Ole Mwarabu Ole Mareka kutoka jamii ya Wamaasai wa Parakuyo iliyoko mjini Morogoro nchini Tanzania alikuwa miongoni mwa washiriki ambao walikuja katika jukwaaa hilo na azimio maalum linalohimiza mama kuvaa kofia yake ili kusaidia kutatua migogoro kuanzia ngazi ya familia, jamii hadi kimataifa. Amezungumza na Flora Nducha wa idhaa hii ya Kiswahili akianza kwa kufafanua kuhusu azimio hilo 

  • 30 APRIL 2024

    30/04/2024 Duración: 12min

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina, Adam Kulet Ole Mwarabu Ole Mareka kutoka jamii ya Wamaasai wa Parakuyo iliyoko mjini Morogoro nchini Tanzania anazungumza na Flora Nducha. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na mashinani.Kamishina Mkuu wa sririka la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA leo amesema watu waliokamatwa wakati wa vita inayoendelea Gaza wamenyanyaswa, kuteswa na kufanyiwa vitendo visivyo vya kibinadamu. Katika taarifa yake iliyotolewa leo mjini Geneva Uswisi Phippe Lazzarini amesema “Watu tuliozungumza nao wametueleza kwamba walipokamatwa kila mara walikuwa wakikusanywa Pamoja, kuvuliwa nguo na kubaki na chupi na kisha kupakiwa katika malori. Watu hawa wametendewa vitendo vya kikatili visivyo vya kibinadamu ikiwemo kuzamishwa kwenye maji na kuumwa na mbwa.”Jahmhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, ndio nchi yenye idadi kubwa ya watu wanaohitaji msaada wa kibinadamu duniani kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la msaada wa kibinadamu na masuala ya dharura OCHA.

  • Wanawake Tanzania wainua wanawake wenzao katika ujasiriamali kupitia mradi wa CookFund

    29/04/2024 Duración: 03min

    Nchini Tanzania mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuendeleza mitaji, UNCDF uitwao CookFund unaofadhiliwa na Muungano wa Ulaya umesaidia wajasiriamali hasa wanawake kuinua wanawake wenzao kwenye sekta ya matumizi ya nishati jadidifu na hivyo kutekeleza ajenda ya 2030 ya Umoja wa Mataifa ya sio tu kuondokana na umaskini bali pia kuhimili na kukabili mabadiliko ya tabianchi.

  • 29 APRILI 2024

    29/04/2024 Duración: 11min

    Hii leo jaridani tunaangazia mzozo na hali ya kibinadamu katika ukanda wa Gaza, na msaada wa kibinadamu nchini Ethiopia. Makala inatupeleka nchini Tanzania na mashinani nchini Somalia, kulikoni? Shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA limeonya hii leo juu ya idadi kubwa ya watoto ambao wako peke yao Gaza, ama wamepoteza wazazo au kutenganishwa nao pamoja na jamaa wa familia pia wakati huu ambapo hawawezi kuhudhuria masomo na shule nyingi zikigeuka kuwa makazi ya wakimbizi wa ndni.Nchini Ethiopia, Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP na wadau wake waanafanya kazi kwa kushirikiana na jamii kutambua wale wenye uhitaji zaidi wa msaada wa kibinadamu, na wananchi wamepongeza WFP kwa mfumo huu mpya wa kutambua wenye uhitaji zaidi.  Makala inakwenda nchini Tanzania kumulika ni kwa vipi mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuendeleza mitaji, UNCDF uitwao CookFund unaofadhiliwa na Muungano wa Ulaya umesaidia wajasiriamali hasa wanawake kuinua wa

  • UNRWA: Watoto 17,000 wametenganishwa na wazazi au familia zao Gaza

    29/04/2024 Duración: 01min

    Shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA limeonya hii leo juu ya idadi kubwa ya watoto ambao wako peke yao Gaza, ama wamepoteza wazazo au kutenganishwa nao pamoja na jamaa wa familia wakati huu ambapo hawawezi kuhudhuria masomo na shule nyingi zikigeuka kuwa makazi ya wakimbizi wa ndni. Kwa mujibu wa tarifa fupi ya UNRWA iliyotolewa kupitia ukurasa wake wa X, shirika hilo linasema maisha ya watoto Gaza yamekuwa jinamizi na takriban 17,000 wako peke yao hawana wazazi au walezi ama wametenganishwa na familia zao.Pia imesema watoto hao wahaudhurii masomo kutokana na vita inayoendelea kwani zaidi ya asilimia 70 ya nyumba zimesambaratishwa au kubomolewa na watoto wengi wamepoteza nyumba zao.UNRWA imeongeza kuwa shule sasa zimelazimika kuwa mkazi ya manusura wa vita hivyo na sio mahala pa elimu tena na kufanya mustakbali wa watoto hao kuwa njiapanda na unahitaji kulindwa.Kutokana na hali mbayá ya hewa na ongezeko la joto UNRWA inasema watu wengi wanhaha hata kupata mahitaji muhi

  • Wananchi nchini Ethiopia wapongeza mfumo mpya wa kutambua wenye uhitaji

    29/04/2024 Duración: 02min

    Nchini Ethiopia Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP na wadau wake waanafanya kazi kwa kushirikiana na jamii kutambua wale wenye uhitaji zaidi wa msaada wa kibinadamu, na wananchi wamepongeza WFP kwa mfumo huu mpya wa kutambua wenye uhitaji zaidi Ethiopia ni moja ya nchi zinazoendelea kukabiliana na athari za mizozo mingi inayoingiliana kama vile ukame, mafuriko pamoja na mizozo. Ili kukabiliana na mahitaji yanayokua WFP na wadau wake wameamua kuanzisha mfumo mpya wa kutambua familia zenye uhitaji zaidi miongoni mwa wanajamii. Mbinu hii inayoendeshwa na wana jumuiya wenyewe inaweka kiwango kipya cha usaidizi wa kibinadamu nchini humo, kama anavyoeleza Mola Suleiman ambaye ni Mshiriki wa Msaada wa WFP anasema, "Wanaotambua wenye uhitaji zaidi sio viongozi, bali watu wasioegemea upande wowote waliochaguliwa na jamii. Tunaweza kwenda kwenye madawati ya usaidizi yaliyoanzishwa huko wilayani Kebeles na viunga vyake na kupeleka malalamiko yetu. Kwa kufuata utaratibu wa uwazi,

  • Mabadiliko ya tabianchi yanachangia katika migogoro katika jamii za asili - Alois Porokwa

    26/04/2024 Duración: 04min

    Mkutano wa 23 wa Jukwaa la Kudumu kuhusu Masuala ya Watu wa Asili, UNPFII uliodumu kwa wiki mbili hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa umefikia tamati leo Aprili 26. Miongoni mwa masuala muhimu yaliyojadiliwa ni mabadiliko ya tabianchi na mazingira, likiwa ni suala ambalo pia miezi miwili iliyopita lilipewa kipaumbele cha juu wakati wa Mkutano wa 6 wa Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa UNEA 6  jijini Nairobi, Kenya. Wakati huo Afisa habari wa kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa jijini Nairobi UNIS, Stella Vuzo alipata fursa ya kuzungumza na Alois Porokwa, Mkurugenzi wa shirika la NALEPPO kutoka jamii ya Wamaasai wa Kijiji cha Emboreet, Wilaya ya Simajiro, Mkoa wa Manyara, Tanzania kuhusu athari za mabadiliko ya tabianchi hususani kwa jamii ambazo bado zinaishi katika mifumo ya asili.

  • Raia Sudan wakumbwa na kihoro kufuatia mapigano kati ya jeshi la serikali na wanamgambo wa RSF

    26/04/2024 Duración: 02min

    Huko nchini Sudan jimboni Darfur Kaskazini, hususan mjini El-Fasher na viunga vyake mapigano kati ya jeshi la serikali SAF na wanamgambo wa RSF yanazidi kuwa na madhara kwa rai ana kumtia hofu kubwa Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu, Volker Türk. Katika kufahamu hali iko vipi, Assumpta Massoi wa Idhaa hii amezungumza na Seif Magango msemaji wa ofisi ya Kamishna Türk kutoka Nairobi, Kenya na anaanza kwa kueleza nini hasa kinamtia hofu Kamishna huyo.

  • 26 APRILI 2024

    26/04/2024 Duración: 12min

    Hii leo jaridani tunaangazia mzozo nchini Sudan, na jinsi amabvyo mzozo huo unavyathiri wanawake. Makala tunaangazia changamoto ya mabadiliko ya tabianchi kwa jamii za watu wa asili na mashinani usafi wa mazingira katika makazi yasiyo rasmi nchini Kenya. Huko nchini Sudan jimboni Darfur Kaskazini, hususan mjini El-Fasher na viunga vyake mapigano kati ya jeshi la serikali SAF na wanamgambo wa RSF yanazidi kuwa na madhara kwa rai ana kumtia hofu kubwa Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu, Volker Türk. Katika kufahamu hali iko vipi, Assumpta Massoi wa Idhaa hii amezungumza na Seif Magango msemaji wa ofisi ya Kamishna Türk kutoka Nairobi, Kenya na anaanza kwa kueleza nini hasa kinamtia hofu Kamishna huyo.Na tukisalia nchini Sudan, mwaka mmoja wa mzozo umewafanya wananchi wengi kukimbia maeneo waliyokuwa wakiishi kusaka hifadhi pamoja na kukimbilia nje ya nchi. Pamoja ya kukimbia vita lakini pia wanasalia na majeraha ndani ya mioyo yao kutokana na masahibu waliyopitia. Mmoja wao ni Bi. Fatima amba

  • Simulizi ya mwanamke aliyebakwa na kupata ujauzito wakati wa mzozo Sudan

    26/04/2024 Duración: 02min

    Mwaka mmoja wa mzozo nchini Sudan umewafanya wananchi wengi kukimbia maeneo waliyokuwa wakiishi kusaka hifadhi pamoja na kukimbilia nje ya nchi. Pamoja ya kukimbia vita lakini pia wanasalia na majeraha ndani ya mioyo yao kutokana na masahibu waliyopitia. Mmoja wao ni Bi. Fatima ambaye alibakwa na kupata ujauzito. Fatima sio jina lake halisi, tunalitumia hili ili kuficha utambulisho wake na hapa anaanza kueleza yale yaliyomsibu akiwa mikononi mwa wanamgambo wenye silaha.“Nilibakwa mara tatu. Aliniambia lala chini, usipotaka kulala chini naweza kukuuwa. Sijui sasa kama ni huyo mwanaume aliniingilia mara tatu au kulikuwa na wengine.” Akiwa na kiwewe na aliyekata tamaa, Fatima akaukimbia mji wake wa Khartoum akiwa na watoto wake kwenda kusini mashariki mwa Sudan, kusaka hifadhi na alipofika huko, anasema “Nilikwenda kuripoti tukio hilo katika kliniki na kusaka msaada ili waweze kunifanyia uchunguzi wa jumla. Nikaenda hospitalini na kila kitu kilikuwa sawa. Baada ya miezi miwili nilienda tena kliniki na

  • Jamii za watu wa asili wanaathiriwa pakubwa na mabadiliko ya tabianchi - Samante Anne

    25/04/2024 Duración: 04min

    Hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa Mkutano wa 23 wa Jukwaa la Kudumu kuhusu Masuala ya Watu wa Asili, UNPFII ukielekea ukingoni huku mambo kadha yakiwa yamejadiliwa kwa wiki mbili na miongoni mwa mambo hayo ni suala la mabadiliko ya tabianchi na mazingira, nilipata fursa ya kuzungumza na mmoja wa washiriki wa jukwaa hilo Samante Anne kutoka shirika lisilo la kiserikali nchini Kenya la Mainyoito Pastoralists Intergrated Development Organization (MPIDO) akieleza namna mabadiliko ya tabianchi yalivyoathiri jamii za watu wa asili nchini mwake.

  • Jifunze Kiswahili: Tofauti ya maneno “Adhimisha na Azimisha.”

    25/04/2024 Duración: 01min

    Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, mchambuzi wetu leo ni Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia tofauti ya maneno “Adhimisha na Azimisha.”

  • 25 APRILI 2024

    25/04/2024 Duración: 10min

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambayo Samante Anne kutoka shirika lisilo la kiserikali nchini Kenya la Mainyoito Pastoralists Intergrated Development Organization (MPIDO) anaeleza namna mabadiliko ya tabianchi yalivyoathiri jamii za watu wa asili nchini mwake. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na neno la wiki. Leo ni siku ya Malaria duniani ambapo mwaka huu inahamasisha kuongeza mapambano dhidi ya ugonjwa huu ili kuwa na ulimwengu wenye usawa zaidi kwani imebainika kuwa watu wanaoishi katika mazingira magumu ndio wanaoathirika zaidi.Leo pia ni siku ya kimataifa ya wasichana katika tehama na mwaka huu inasherehekea uongozi ikisisitiza hitaji muhimu la kuwa na mifano thabiti ya wanawake viongozi katika taaluma ya sayansi, teknolojia, uhandishi na hisabati -STEM kwani hali ilivyo sasa kuna wanawake viongozi wachache katika maeneo hayo.  Na tukisalia na masuala ya wasichana katika tehama Shirika la Umoja Wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni UNESCO limetoa ripoti inayoonya kuwa pamoja na faida za

  • Watoa chanjo wavuka mabonde na mito kufikisha chanjo kwa walengwa Tanzania

    24/04/2024 Duración: 03min

    Wiki ya kimataifa ya chanjo ikifungua pazia, nchini Tanzania wahudumu wa afya kama Prisca Mkungwa wanajitoa kwa kadri ya uwezo wao kuhakikisha huduma za chanjo zinafikia walengwa wote hata wale walioko maeneo ya mbali. Mathalani huko wilayani Chunya, mkoani Mbeya, kusini magharibi mwa taifa hilo ambako kupitia ushirikiano na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, chanjo dhidi ya surua inatolewa kwa watoto. Prisca na wenzake kutokana na kupenda kazi yao wanafanya kila njia iwe ni kutumia usafiri wa bodaboda au hata kuvuka mito na mabonde kwa miguu kuhakikisha chanjo zinafika. Kufahamu kwa kina ungana na Assumpta Massoi katika makala hii iliyoandaliwa na UNICEF Tanzania.

  • Wiki ya Chanjo Duniani yaanza leo 24 hadi 30 Aprili 

    24/04/2024 Duración: 01min

    Leo ni siku ya kwanza ya siku saba za Wiki ya Chanjo Duniani.(Taarifa ya Anold Kayanda)Wiki ya Chanjo Duniani ambayo huadhimishwa katika kila wiki ya mwisho ya mwezi Aprili, inalenga kuangazia hatua za pamoja zinazohitajika na kuhimiza matumizi ya chanjo kuwalinda watu wa rika zote duniani dhidi ya magonjwa.Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni, WHO linashirikiana na nchi kote ulimwenguni kuhamasisha ufahamu wa thamani ya chanjo na uchanjaji na kuhakikisha kuwa serikali zinapata mwongozo unaohitajika na usaidizi wa kiufundi ili kutekeleza programu za uchanjaji zenye ubora wa hali ya juu.Lengo kuu la Wiki ya Chanjo Duniani ni kwa watu zaidi  na jamii zao kulindwa dhidi ya magonjwa yanayoweza kuzuilika.WHO inasema chanjo zimesaidia sana ikitolea mfano namna ulimwengu umeweza kutokomeza ugonjwa wa ndui ambapo mtu wa mwisho kuugua ugonjwa huo ni miaka 47 iliyopita.Mwaka huu Wiki ya Chanjo Duniani inaadhimisha miaka 50 ya EPI ambao ni mpango ambao WHO iliuanzisha mwaka 1974 kwa lengo la kufanya chanjo zi

  • Mtu 1 kati ya 5 katika nchi 59 duniani anahitaji hatua za haraka kuepushwa na baa la njaa: FAO

    24/04/2024 Duración: 02min

    Ripoti mpya ya kimataifa iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO kuhusu mgogoro wa chakula duniani inasema karibu watu milioni 282 walio katika nchi 59 walikabiliwa na viwango vya juu vya njaa mwaka 2023. (TAARIFA YA FLORA NDUCHA)Asante Leah. Kwa hakika ripoti hiyo ya “Mgogoro wa kimataifa wa chakula” GRFC inasema kiwango cha watu wenye njaa duniani kiliongezeka kwa watu milioni 24 kutoka mwaka 2022 hadi 2023 na ni asilimia 21.5 ya watu waliofanyiwa tahimini  na hicho ni kiwango kikubwa sana ukilinganisha na ilivyokuwa kabla ya janga la COVID-19 limesema shirika la FAO likiongeza kuwa idadi ya walio na njaa duniani inaendelea kuongezeka.Ripoti imetaja sababu kuu tatu ambazo zinachangia kwa kiasi kikubwa janga la njaa duniani ambazo ni mosi migogoro na vita ambapo inasema inaathiri katika nchi 20 zilizo na jumla ya watu milioni 135 wanaokabiliwa na njaa zikiwemo Sudan, Yemen na Palestina katika Ukanda wa Gaza.Pili ni matukio mabaya ya hali ya hewa yaliyochangiwa na mabadiliko ya

  • 24 APRILI 2024

    24/04/2024 Duración: 10min

    Karibu kusikiliza jarida hii leo linaangazia masuala mbalimbali ikiwemo ripotoi ya mgogoro wa chakula duniani, kuanza kwa wiki ya chanjo na utoaji chanjo kwa watoto mashinani. 

página 5 de 5