Sinopsis
Makala yanayochambua masuala na matukio mbalimbali yaliyotokea kwenye jamii kwa wiki nzima kwa kina, yanatoa fursa kwa msikilizaji kueleza hisia na mtazamo wake juu ya masuala yanayoendelea kutokea iwe ni katika uga wa uchumi na siasa duniani kote.
Episodios
-
DRC na waasi wa M23 kukubaliana kuhusu amani ya mashariki, Humphrey polepole akosoa CCM
19/07/2025 Duración: 20minSerikali ya Kinshasa na waasi wa AFC/M23 mbioni kusaini makubaliano ambayo kimsingi yanaleta matumaini ya kufikia amani mashariki mwa nchi hiyo, Tanzania yazindua dira ya maendeleo 2050 kuelekea uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba, umoja wa mataifa wasema hali ya kibinadamu nchini Sudan si ya kuridhisha, rais Paul Biya, kiongozi mkongwe sana duniani na umri wa miaka 92 kuwania urais kwa muhula wa nane, umoja wa ulaya kutishia kuiwekea Urusi vikwazo vipya na hali ya nchini Syria
-
Rais Ruto aibua hisia kali kwa kuwaagiza polisi kuwapiga risasi ya miguu waandamanaji
12/07/2025 Duración: 20minWiki hii watu wasiopungua 38 waliuawa nchini Kenya kufuatia maandamano ya SabasAba siku ya Jumatatu. Rais Ruto aliibua hisia kali alipowaagiza polisi kuwapiga risasi ya miguu waandamanaji. Lakini pia, malalamiko yaliwasilishwa rasmi huko Brussels, dhidi ya wanafamilia tisa wa rais wa DRC Félix Tshisekedi, ambao wana uraia wa Ubelgiji, wakituhumiwa kwa wizi wa madini ya nchi yao. Tutakujuza pia taarifa za kikao cha Rais wa Marekani Donald Trump na marais sita wa Afrika magharibi kilichofanyika, lakini pia Uingereza na Ufaransa kutangaza rasmi mpango wa majaribio wa kuwarudisha Paris baadhi ya wahamiaji wanaowasili nchini humo kwa kutumia boti ndogo.
-
Rais Kagame na Makubaliano ya Washington DC na mazishi ya Albert Ojwang Kenya
05/07/2025 Duración: 20minYaliyoangaziwa katika makala hii ni pamoja na kauli ya rais wa Kenya kujenga kanisa ndani ya ikulu ya Nairobi, rais Paul Kagame wa Rwanda na mkataba wa amani ulioisainiwa kati ya nchi yake na DRC, waziri mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa kutogombea tena ubunge kuwakilisha jimbo la Ruangwa, hali nchini DRC, Sudan na kauli ya Ufaransa kuwa inatarajia Algeria kumsamehe mwandishi wa vitabu Boualem Sansal aliyefungwa, lakini pia mkutano wa viongozi wa Ulaya kule London Uingereza kufanyika wiki ijayo
-
Maandamano mapya yaua 16 Kenya, DRC na Rwanda zasaini makubaliano ya amani
28/06/2025 Duración: 20minWiki hii ulimwengu umeshuhudia matukio mengi ya ajabu na hatari sana kwa usalama wa nchi mbali mbali, kwanza nchini Kenya watu 16 waliuawa katika maandamano ya kuadhimisha mwaka mmoja wa mauaji ya vijana Gen Z, Rwanda na DRC zatia saini mkataba wa amani kumaliza vita vya mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, siasa za Chad, Zambia na pia mashambulizi kati ya Israeli na Iran, pamoja na mkutano wa jumuia ya NATO..na mengine mengi