Sinopsis

Makala haya yanaangazia maendeleo ya michezo mbalimbali Ulimwenguni na pia huwa haiwaweki kando wanamichezo waliobobea na vilevile kufanya uchanganuzi wa kina wa michezo wakati wa mashindano mbalimbali. 

Episodios

 • Jukwaa la Michezo - Rais wa Fifa apendekeza fainali za Afrika kuchezwa baada ya miaka minne

  Jukwaa la Michezo - Rais wa Fifa apendekeza fainali za Afrika kuchezwa baada ya miaka minne

  04/02/2020 Duración: 16min

  Rais wa shirikisho la kandanda duniani Fifa Gian Infantino amependekeza fainali za mataifa ya Afrika kuchezw akila baada ya miaka minne badala ya miaka miwili ya sasa. Tunajadili kwa kina katika jukwaa la michezo. Ungana na Fredrick Nwaka akiwa na wachambuzi wa soka Mustapha Mtupa, Samwel John na Bonface Osano

 • Jukwaa la Michezo - TP Mazembe, Mamelody Sundowns zafuzu robo fainali ya klabu bingwa Afrika

  Jukwaa la Michezo - TP Mazembe, Mamelody Sundowns zafuzu robo fainali ya klabu bingwa Afrika

  27/01/2020 Duración: 15min

  Michuano ya klabu bingwa barani Afrika hatua ya makundi imeendelea kurindima ambapo klabu za TP Mazembe, Mamelody Sundowns, Zamalek ni miongoni mwa klabu zilizofuzu hatua ya robo fainali. Je msisimko wa michuano hiyo umepungua msimu huu? Fredrick Nwaka ameungana na wachambuzi wa soka Mohammed Simbaulanga na Aloyce Mchunga kutathimini kwa kina.  

 • Jukwaa la Michezo - Fainali za Afrika 2021 kuchezwa mwezi Januari hadi Februari

  Jukwaa la Michezo - Fainali za Afrika 2021 kuchezwa mwezi Januari hadi Februari

  20/01/2020 Duración: 24min

  Shirikisho la kandanda Afrika CAF wiki hii lilitangaza kubadili ratiba ya fainali za Afrika za mwaka 2021 zitakazochezwa nchini cameroon kutoka Juni hadi Januari. Uamuzi huu una tija? Ungana na Fredrick Nwaka akiwa na wachambuzi wa soka Bonface Osano na Samwel John kutathimini kwa kina.

 • Jukwaa la Michezo - Changamoto na mafanikio ya soka nchini Rwanda

  Jukwaa la Michezo - Changamoto na mafanikio ya soka nchini Rwanda

  13/01/2020 Duración: 21min

  Mchezo wa soka unapendwa na kufuatiliwa kwa kariubu nchini Rwanda hata hivyo taifa hilo la Afrika mashariki bado halijapiga hatua kubwa katika mchezo huo. Tunaangazia mafanikio na changamoto za soka nchini Rwanda. Ungana na Fredrick Nwaka akiwa na Christopher Karenzi, mchambuzi na mwandishi wa habari za spoti kutoka Rwanda

 • Jukwaa la Michezo - Matukio makubwa yatakayotokea viwanjani mwaka 2020

  Jukwaa la Michezo - Matukio makubwa yatakayotokea viwanjani mwaka 2020

  06/01/2020 Duración: 23min

  Leo katika Makala ya Jukwaa la Michezo, tunakuletea baadhi ya matukio makubwa yatakayotokea viwanjani mwaka 2020, ikiwa ni pamoja na tuzo la mchezaji bora katika mchezo wa soka barani Afrika, fainali ya CAF Super Cup na michuano ya CHAN, bila kusahau mashindano ya riadha ya dunia mwaka 2020 nchini Kenya.

 • Jukwaa la Michezo - Matukio makubwa ya michezo yaliyojiri Afrika mashariki 2019

  Jukwaa la Michezo - Matukio makubwa ya michezo yaliyojiri Afrika mashariki 2019

  30/12/2019 Duración: 23min

  Eneo la Afrika mashariki mwaka 2019 limeshuhudioa matukio mbalimbali ya spoti yaliyogusa hisia ya wapenzi wa michezo. Tunayaangazia kwa kina katika makala ya jukwaa la michezo.

 • Jukwaa la Michezo - Viongozi wapya wa Cecafa wana jukumu zito kuinua mchezo wa soka

  Jukwaa la Michezo - Viongozi wapya wa Cecafa wana jukumu zito kuinua mchezo wa soka

  23/12/2019 Duración: 23min

  Wiki hii baraza la vyama vya soka kwa nchi za Afrika mashariki na kati Cecafa limepata viongozi wapya akiwemo rais mpya Wallace Karia. Viongozi hao wataongoza shirikisho la soka kwa kipindi cha miaka minne ijayo. Ungana na Victor Abuso, Fredrick Nwaka na Bonface Osano wakijadili kwa kina

 • Jukwaa la Michezo - Michuano ya CECAFA 2019 yaanza nchini Uganda

  Jukwaa la Michezo - Michuano ya CECAFA 2019 yaanza nchini Uganda

  10/12/2019 Duración: 23min

  Makala ya 40 kutafuta ubingwa wa mchezo wa soka katika nchi za Afrika Mashariki na Kati, yamefungua milango yake jijini Kampala nchini Uganda. Pamoja na hillo, michuano ya klabu bingwa barani Afrika, hatua ya makundi inachezwa katika viwanja mbalimbali barani Afrika.Tunachambua matukio haya mawili, miongoni mwa mengine.

 • Jukwaa la Michezo - Umuhimu wa kuinua soka la wanawake katika ukanda wa Cecafa

  Jukwaa la Michezo - Umuhimu wa kuinua soka la wanawake katika ukanda wa Cecafa

  02/12/2019 Duración: 23min

  Michuano ya Cecafa kwa wanawake imemalizika nchini Tanzania kwa Kenya kutwaa ubingwa. Mwandishi wa spoti Fredrick Nwaka amefanya mazungumzo na Naibu rais wa shirikisho la kandanda nchini Kenya kuangazia mafanikio ya soka la wanawake nchini Kenya na katika ukanda mzima wa Cecafa.

 • Jukwaa la Michezo - Cecafa inanuia kupeleka timu ya wanawake kombe la dunia

  Jukwaa la Michezo - Cecafa inanuia kupeleka timu ya wanawake kombe la dunia

  26/11/2019 Duración: 20min

  Mashindano ya vyama vya soka kwa nchi za Afrika mashariki na kati yanafanyika nchini Tanzania ambapo RFI Kiswahili kupitia kipindi cha Jukwaa la Michezo imepata fursa ya kuzungumza na katibu mkuu wa Cecafa Nicholas Musonye. Ungana na Fredrick Nwaka kwa undani zaidi

 • Jukwaa la Michezo - Michezo ya kufuzu fainali za Afrika zaendelea kurindima

  Jukwaa la Michezo - Michezo ya kufuzu fainali za Afrika zaendelea kurindima

  18/11/2019 Duración: 21min

  Michuano ya kuwania kufuzu fainali za Afrika imekuwa ikichezwa katika viwanja mbalimbali barani Afrika huku Uganda iking'ara, nayo Kenya ikitaraji kuipokea Togo mjini Nairobi. Ungana na Victor Abuso na Fredrick Nwaka viwanjani.

 • Jukwaa la Michezo - Kwanini hamasa ya mchezo wa wapinzani wa jadi nchini Kenya umepungua?

  Jukwaa la Michezo - Kwanini hamasa ya mchezo wa wapinzani wa jadi nchini Kenya umepungua?

  11/11/2019 Duración: 24min

  Gor Mahia imeishinda AFC Leopards kwa mabao 4-1 katika mchezo wa upande mmoja wa wapinzani wa jadi nchini Kenya. Hata hivyo msisimko wa soka nchini Kenya umepungua miaka ya karibuni kutokana na kukosekana kwa hamasa ya mchezo baina ya wapinzani wa jadi. Fredrick Nwaka ameungana na wachambuzi wa soka Bonface Osano na Aloyce mchunga kutathimini kwa kina.

 • Jukwaa la Michezo - Klabu za Afrika Mashariki na Kati zashindwa kuwika katika michuano ya Shirkisho barani Afrika

  Jukwaa la Michezo - Klabu za Afrika Mashariki na Kati zashindwa kuwika katika michuano ya Shirkisho barani Afrika

  04/11/2019 Duración: 23min

  Klabu za  soka kutoka ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, zipo mbioni katika michuano ya mzunguko wa mwisho, kufuzu katika hatua ya makundi, kuwania taji la Shirikisho barani Afrika, lakini pia tunaangazia kujiuzulu kwa Katibu Mkuu wa chama cha Riadha nchini Tanzania  Wilhelm  Gidabuday.

 • Jukwaa la Michezo - Fifa yakabiliwa na shutuma kwa kuipa China uandalizi wa klabu bingwa ya dunia

  Jukwaa la Michezo - Fifa yakabiliwa na shutuma kwa kuipa China uandalizi wa klabu bingwa ya dunia

  28/10/2019 Duración: 21min

  Shirikisho la kandanda duniani Fifa linakabiliwa na shutuma kali kwa kuipatia China uandalizi wa mashindano ya klabu bingwa ya dunia 2021 na michuano ya kombe la shirikisho yaendelea, Yanga na Gor Mahia zachechemea. Fredrick Nwaka ameungana na wachambuzi Samwel John na Anangisye Msokwa kukuletea makala haya.

 • Jukwaa la Michezo - Tanzania, Uganda na Rwanda yafuzu fainali ya CHAN 2020

  Jukwaa la Michezo - Tanzania, Uganda na Rwanda yafuzu fainali ya CHAN 2020

  21/10/2019 Duración: 24min

  Mataifa ya Tanzania, Uganda na Rwanda yamefuzu katika fainali ya CHAN kwa wachezaji wanaocheza soka barani Afrika mwaka 2020. DRC nayo pia imefuzu. Michuano hiyo itafanyika nchini Cameroon. Tunajadili michuano hii na maandalizi ya mataifa ya Afrika Mashariki.

 • Jukwaa la Michezo - Ligi kuu ya soka nchini Kenya yakabiliwa na changamoto za fedha

  Jukwaa la Michezo - Ligi kuu ya soka nchini Kenya yakabiliwa na changamoto za fedha

  14/10/2019 Duración: 21min

  Ligi kuu ya soka nchini Kenya, inakabiliwa na changamoto za kifedha, baada ya mfadhili mkuu SportPesa kujiondoa.Hali hii imesababisha baadhi ya klabu kushindwa kuwalipa wachezaji wake mishahara. Changamoto hii inaweza kutatuliwa vipi ? Ungana na Fredrick Nwaka na wageni wetu.

 • Jukwaa la Michezo - Tanzania Bara yanyakua taji la michuano ya vijana ya Cecafa nchini Uganda

  Jukwaa la Michezo - Tanzania Bara yanyakua taji la michuano ya vijana ya Cecafa nchini Uganda

  07/10/2019 Duración: 23min

  Michuano ya Cecafa kwa vijana chini ya miaka 20 imetamatika nchini Uganda kwa tanzania Bara kushinda ubingwa huo kwa kuitandika Kenya bao 1-0. Hata hivyo mashindano hayo yamegubikwa na madai ya udanganyifu wa umri wa wachezaji na vilevile ushiriki hafifu wa baadhi ya nchi. Nini hatima ya soka la vijana baada ya mashindano haya? Fredrick Nwaka ameungana na mchambuzi wa soka Samwel John na Naibu rais wa shirikisho la kandanda nchini Kenya FKF Doris Petra kutathimini kwa kina.

 • Jukwaa la Michezo - Gor Mahia, Yanga na KCCA zaondolewa klabu bingwa Afrika

  Jukwaa la Michezo - Gor Mahia, Yanga na KCCA zaondolewa klabu bingwa Afrika

  30/09/2019 Duración: 22min

  Michuano ya klabu bingwa Afrika imeendelea mwishoni mwa juma huku Gor Mahia, Yanga na KCCA zikiondolewa katika michuano ya klabu bingwa Afrika na mashindano ya riadha ya Doha Marathon yakumbwa na changamoto ya joto kali. Tunajadali haya katika jukwaa la michezo. Ungana na Fredrick Nwaka akiwa na wachambuzi wa michezo Aloyce Mchunga na Bonface Osano

 • Jukwaa la Michezo - Historia ya kituo cha michezo cha Alliance kilichopo Mwanza, kaskazini magharibi mwa Tanzania

  Jukwaa la Michezo - Historia ya kituo cha michezo cha Alliance kilichopo Mwanza, kaskazini magharibi mwa Tanzania

  23/09/2019 Duración: 24min

  Makala ya Jukwaa la Michezo Jumapili ya Septemba 22, 2019 imeangazia historia, mafaniko na changamoto ambazo kituo hicho kinakabiliana nazo. Ungana na fredrick Nwaka akizungumza na Yusuph Budodi mwenyekiti wa kamati ya mashindano kituoni hapo.

 • Jukwaa la Michezo - Yanga, Gor Mahia zashindwa kuchanua klabu bingwa Afrika

  Jukwaa la Michezo - Yanga, Gor Mahia zashindwa kuchanua klabu bingwa Afrika

  16/09/2019 Duración: 22min

  Michuano ya klabu bingwa Afrika na Kombe la shirikisho imekuwa ikichezwa mwishoni mwa wiki hii huku klabu za Afrika Mashariki na Kati kama Yanga na Gor Mahia zikishindwa kufanya vyema. Tunatathimi ni kwa kina mashindano haya. Ungana na Fredrick Nwaka akiwa na wachambuzi wa kandanda Aloyce Mchunga na Bonface Osano.

Informações: