Habari Za Un

Mashirika ya UN yaonya kuwa maelfu ya maisha ya watu El Fasher Sudan yako hatarini

Informações:

Sinopsis

Mashirika ya misaada ya Umoja wa Mataifa leo yameonya kwamba maisha ya maelfu ya watu yako hatarini El Fasher Sudan, kufuatia mashambulizi makali yanayoendelea ambapo moja ya hospitali Darfur Kaskazini imeshambuliwa na kukatili maisha ya watu wawili lakini pia kuchochea hofu ya kurejea kwa baa la njaa. Kwa mujibu wa Mratibu wa misaada ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa Martin Griffiths, “Shambulio hilo limeharibu paa la hospitali katika kituo cha huduma za dharura kwenye Hospitali ya Sourthen katika mji wa El Fasher ambayo ndio hospitali pekee inayofanyakazi kwas asa katika jimbo la Darfur Kaskazini na ambako vifaa vya matibabu na dawa sasa karibu vinakwisha.” Amesema takriban watu 800,000 wanaishi katika mji wa El Fasher na maelfu ya maisha yao yako hatarini huku taifa zima la Sudan likiwa katika hali mbaya.Shirika la kuratibu misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura OCHA limesema makumi ya raia waliuawa mwishoni mwa wiki katika mapigano mapya  makubwa yaliyozuka Ijumaa kati ya vikosi vya se